Murathe na Siasa za 2022

Baada ya matamshi yake naibu mwenyekiti wa chaa cha Jubilee David Murathe ya kuwaambia wananchi wanapaswa kujitayarisha kumlaki kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kama rais wa Kenya baadhi ya wanachama wake walitaka aadhibiwe kwa kumpigia debe kinara huyo.

Miongoni mwa wale ambao wanaotaka mwanasiasa huyo aadhibiwe ni Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa.

Barasa alishangazwa ni kwa nini Murathe hajachukuliwa hatua yeyote kwa maana yeye ni kiongozi ilhali anampigia mwanachama wa chama kingine debe.

Mbunge wa Nyeri Town, Ngunjiri Wambugu, ambaye ni mwanachama wa mrengo wa kieleweke alichangia mjadala huo kwa kusema Murathe alikuwa anaendesha kampeni kulingana na maagizo ya rais. Seneta wa Nandi, Samson Cherargei alitaja matamshi ya Murathe kama ya kumhakikishia Raila kuungwa mkono na Mlima Kenya kufuatia matamshi ya Irungu Kang’ata kuhusu ugavi wa mapato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *