Je, Bunge la Seneti litaitikia wito kutoka kwa serikali za Kaunti?

Changamoto inazidi kutolewa kwa bunge  la seneti na serikali kuu kusaka mwafaka kuhusiana na mgogoro wa ugavi wa mapato  kwa serikali za kaunti nchini.

Viongozi wa serikali ya kaunti Baringo wakiongozwa na wawakilishi wadi pamoja na viongozi wa bunge la  kaunti hiyo  chini ya mwenyekiti wao Francis Koech  ambaye ni  karani  wa bunge la kaunti hiyo amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba  kaunti hazikosi fedha na hivyo kuhujumu huduma  kwa wananchi kutokana na mgogoro huo.

Amemtaka rais Uhuru Kenyatta kusimama kidete na kuhakikisha ya kwamba hamna muingilio wowote wa kisiasa ila iwafaidi wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *