Askofu Kimengich amtembelea na Gavana Mandago

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret askofu Dominic Kimengich, amefanya ziara ya kumtembelea gavana wa kaunti ya Uasin gishu JacksonĀ  Mandago ili kutoa shukran kwenye hafla ya kutawazwa kwake kama askofu.

Kwenye hafla hio iliofanyika katika makao makuu ya kaunti, askofu Kimengich amemzawadi gavana Mandago biblia ya lugha ya kikalenjin na kitabu cha Tumshangilie Bwana.

Wakti huo pia askofu ameshukuru gavana kwa kazi nzuri walioifanya kama kaunti wakati wa kumuaga aliyekuwa askofu wa jimbo hili mtangulizi wake marehemu askofu Cornelius Korir.

Kando na hayo askofu kwenye ziara hio pia ametakawaweze kushirikiana katika shughuli za kuendeleza gurudumu la afya kwenye kaunti. Padre Fredrick Njoroge vilevile alihudhuria kikao hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *