Ipo haja ya vijana kupewa nasaha na mawaidha ya jinsi maisha ilivyo bila ya kuwapuuza kwa kuwa hili hupelekea maafa yanayotokana na wao kushindwa na hali ya Maisha.
Ni kauli yake kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Abdirisak Jaldesa ambaye anasema vipo visa vingi ambavyo havijapata kuripotiwa vya vijana kujitoa uhai kwa kushindwa na jinsi watakavyoendeleza maisha yao.
Kamishna huyo ameyasema haya Mjini Eldoret wakati na ambapo kuliripotiwa hiyo jana mwanamme Mmoja mwenye umri wa miaka 20 alijitoa uhai kwa kukosa ujira, swala analosema kama kijana huyo angetafuta mawaidha kutoka kwa kikundi cha rika yake labda hangechukua hatua hiyo. Halikadhalika, Jaldesa amesema vijana katika kaunti hiyo Sasa watakua wanapokea mawaidha na mafunzo ya kujikimu kimaisha kila baada ya siku 11.