Kesi ya Khalwale yatupiliwa mbali

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ameondoa mashtaka ya uchochezi dhidi ya aliyekuwa Seneta wa Kakamega Boni Khalwale.

Khalwale alitarajiwa kufika kortini asubuhi Ijumaa, Juni 12 kujibu mashtaka ya uchochezi na kuandaa mkutano kinyume na maagizo ya serikali ya kudhibiti COVID-19. Lakini, wakili wake Dantan Omari aliwaambia waandishi wa habari kwamba DPP ametupilia mbali mashtaka dhidi ya mteja wake.

Polisi walidai kuwa mnamo Juni 5,2020 katika Kijiji cha Mugomari eneo bungle la Mugomari mashariki, Kakamega, aliandaa mkutano wa hadhara na kuanza kuwahutubia wakazi.

Kando na hayo alikabiliwa na tuhuma za kutoa matamshi ya kuzua vurugu ambapo inadaiwa aliwachochea vijana kuwafurusha Waziri na gavana waliokuwa wakitoa msaada wa chakula kwa wakazi. Khalwale alijisalimisha katika afisi za Upelelezi eneo la Kakamega Kusini muda mfupi baada ya agizo la kukamatwa kwake kutolewa Jumatano. Aliachiliwa kwa dhamana ya KSh 200,000 muda mfupi baada ya kuandikisha taarifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *