Taifa la Kenya hii leo linajiunga na mataifa mengine kote ulimwenguni ili kuadhimisha ugonjwa wa nasuri au kwa lugha ya kimombo kama fistula.
Wakti huo takwimu zinaashiria kuwa zaidi ya wanawake 350,000 humu nchini waugua kutokana na maradhi hayo huku idadi ya wale wanaofika katika hospitalini ili kupokea matibabu ikiwa ni ya chini mno.
Itakumbukwa kuwa ugonjwa huo wa fistula hupatikana wakti mwanamke anapojifungua na kuibuka tatizo wakti wa kumtoa mtoto huyo.
Fikra potovu au kasumba miongoni mwa jamii wakihusisha ungonjwa huo na umaskini huku ikikdariwa kuwa wanawake wapatao 7,000 huathirika kutokana na ugonjwa huo wa fistula kila mwaka hapa nchini pekee.