Rais Kenyatta awapa vijana matumaini ya ajira

Mapema hii leo kiongozi wa taifa rais Uhuru Kenyatta Amesema kupitai mpango wa Kazi Mtaani, vijana wengi nchini wameajiriwa na serikali katika chini ya kauli mbiu hiyo ili kusafisha miji yote nchini.

Ameongezea kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 5 ili kufaniskisha uzalishaji wa bidhaa za humu nchini na kuinua maisha ya mkenya wa kawaida.

Kenyatta amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuangazia jinsi ya kurejelea shughuli za masomo nchini. Kufuatia swala hilo hilo la elimu, Kenyatta amesema wataajiri walimu kote nchini ili kufanikisha masomo kupitia dijitali.

Hazina ya kitaifa imetenga shilingi bilioni 30 kwa minajili ya kurekebisha njia zote zilizoaribika nchini. Kenyatta vilevile amesema serikali imetenga mikakati murwa ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo nchini.

Ameelezea kuwa serikali vilevile itawaajira wahudumu wa afya kutoka kwa kitengo cha stashahada na shahada ili kufanikisha shiughuli za matibabu.

Kuhusiana na sekta za Utafiti nchini, Kenyatta amesema serikali imetenga pesa za kutosha ili kufanikisha utafiti katika idara hizo.

Kuhusiana na kilimo, rais Uhuru amesema serikali itahaklikisha imepunguza bei ya mbolea ili kuwapa wakulima wakati wa kujianda kwa upanzi.

Bilioni 1.5 zimetengewa wakulima wa kilimo cha mauwa nchini ili kujikimu kimaisha baada ya biashara zao kusitishwa kutokana na hatua ya serikali nyingi kufunga shughuli za usafiri.

Wizara ya Utalii nchini imetengewa shilingi bilioni moja kama njia ya kuinua kiwango cha Utalii nchini ambacho kimeathirika pakubwa.

Serikali imetenga shilingi milioni 600 ili kufanikisha ununuzi wa vifaa ambavyo vinatengenezwa nchini chini ya kauli mbiu buy kenya build Kenya.

Kenyatta ameirai bunge la kitaifa kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka huu ili kufanikisha maisha ya mkenya wa kawaida. Wakti huo Shilingi bilioni 1.7 zimetengwa kwa minajili ya kupanua hospitali za humu nchini.

Kiongozi wa taifa amesema kuwa serikali pia imetenga bilioni 10 ili kulipa madeni yake yote. Amewatakia waislamu wote siku njema ya kufungua mfungo wa Ramadhan japo akawakumbusha kuheshimu masharti yaliwekwa na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *