Watu 31 zaidi wamepatwa na virusi vya corona chini ya saa 24 na kufikisha idadi ya watu walioathirika kufika 1,192.
Taarifa hiyo ilitolewa na Rais Uhuru Kenyatta hii leo wakati wa kuhutubia taifa katika Ikulu.
Rais Kenyatta amesema kufikia sasa, taifa limewapima watu 57,650 kote nchini.
Wakati uo huo Kenyatta amesema serikali yake imetenga milioni 250 kwa minajili ya watu walio na mahitaji spesheli na ambao wameathirika pakubwa kutokana na janga la corona.
Rais alisema ugonjwa huo wa covid-19 umeathiri pakubwa uchumi wa Kenya lakini serikali inajikakamua kuhakikisha hali inadhibitiwa.
Kenyatta amewataka wakenya kuendelea kushirikiana na serikali kama njia ya kuangamiza kabisa janga la corona