Mafuriko Elgeiyo Marakwet

Kwa muda sasa idara ya utabiri wa hali ya hewa imekuwa ikitoa taarifa kuhusiana na mvua kubwa ambayo inatarajiwa kuendelea kunyesha nchini kwa muda.

Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini,baadhi ya kaunti zimeathirika pakubwa kutokana na mvua hiyo inayoendelea kunyesha huku maelfu ya watu wakiwa wameachwa bila makao.

Baadhi wameripotiwa kuaga dunia baada ya kusombnwa na mafuriko yanayoshuhudiwa sehemu mbali mbali nchini.

Kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini na haswa kaunti za Rift Valley, Maelfu ya wakenya wanaendelea kuhama makwao kutokana na athari kubwa inayosababishwa na mvua hiyo kubwa.

Kwa sasa katika kaunti ya Elgiyo Marakwet watu 28 wameripotiwa kuaga dunia kutokana na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa katika kaunti hiyo, idadi ambayo gavana wa kaunti hiyo Alex Tolgos. Kaunti jirani za Pokot Magharibi na nyinginezo pia zimeathirika pakubwa huku ikisemekana kuwa huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka .

Tolgos ameongeza kuwa familia nyingi zimelazimika kupiga kambi katika shule za msingi za Sambalat na Wewa .Serikali kuu,kaunti zinapakana na eneo hilo na wasamaria wema wamelazimika kupeleka misaada eneo hilo kutokana na madhara makubwa yaliyosababishwa na virusi hivyo. Mwenyekiti wa bodi ya magavana nchini Wyclife Oparanya ambaye pia ni gavana wa Kakamega , alituma risala ra rambi rambi kwa jamaa waliowapoteza wapendwa wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *