katibu mkuu wa chama cha walimu knut tawi la chepkoilel kaunti ya uasin gishu sammy bor ameunga mkono pendekezo la serikali la kutaka kutumia shule kuwatenga waathiriwa wa virusi vya corona.
akiongea na kituo hiki kupitia kwa njia ya simu katibu huyo amesema ya kwamba ni vyema kila mtu kuajibika na kushirikiana katika vita dhidi ya virusi hatari vya corona. amesisitiza kuwa janga hili ni la taifa nzima kwa hivyo hana budi kuunga mkono mapendekezo yatakayosaidia katika vita dhidi ya virusi hivyo.
haya yanajiri wakati gavana wa kaunti ya elgeyo alex tolgos akiwa ameshatenga baadhi ya shule katika kaunti hiyo kutumika na waathiriwa wa virusi vya corona iwapo watapatikana.