Watu wawili walazwa kutokana na mlipuko wa gesi, maili nne-Eldoret.

Watu wawili kwa sasa wanauguza majeraha ya moto kwenye Hospitali ya mafunzo na rufaa ya hapa mjini Eldoret kutokana na mkasa wa kilipuka kwa gesi.

Wawili hao ambao ni wanaume wanadaiwa kukumbana na majeraha hayo baada ya mtungi wa gesi kulipuka katika mtaa wa maili nne hapa mjini Eldoret kwenye kaunti hii ya Uasingishu.

Mkasa huo unaarifiwa kutokea hii baada ya mtu mmoja kujaribu kuufunguwa mtungi huo, kabla ya kulipuka na kugonga taa ya stima eneo hilo tukio lililofanya moto huo kusambaa kwa kasi mno. Yakijiri hayo ni kuwa wenyeji wa eneo hilo sasa wanainyoshea kidole cha lawama baadhi ya makampuni ya kuuza mitungi ya gesi, kwa kukosa kutoa maelekezo au hamasisho kwa wananchi kuhusu mbinu mwafaka za kutumia mitungi hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *