Nyagah; Si Vizuri Wakenya Kuhangaishwa Uchina

Aliyekuwa waziri Joe Nyagah ameelezea kutoridhishwa kwake na jinsi serikali ya Kenya inavyoshughulikia suala ya wakenya kuhangaishwa nchini Uchina.

Nyagah amesema serikali imewafeli waathiriwa wanaojumuisha raia wengine wa mataifa ya bara Africa ambao wamekuwa wakifurushwa kwenye nyumba zao kwa madai ya kusambaza upya virusi vya corona.

Waziri huyo wa zamani ambaye ni mshauri wa rais Uhuru Kenyatta kuhusu masuala ya uwiano na utangamanao wa kimaeneo, amesema kutochukuliwa kwa hatua  mahususi kuhusu suala kutachangia pakubwa visa vya kulipiza kisasi kwa raia wa Uchina wanaoishi katika mataifa ya bara la Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *