Nairobi sasa ni chini ya Serikali Kuu

Baraza la magavana kwa sasa limeidhinisha mkataba ambapo serikali ya kitaifa itasimamia utoaji wa huduma kwa wakaazi kwenye kaunti ya Nairobi.

Mwenyekiti wa baraza hilo amesema kuwa hatua hio ya gavana sonko itahakikisha kuwa kaunti ya Nairobi inaendelea kutoa huduma kwa wakaazi na wakenya kwa ujumla bila kusita.

Wakti huo ametaja uwepo wa makao makuu ya mashirika makuu ya kimataifa miongoni mwao ikiwemo shirika la umoja wa mataifa ikiwa ni sababu kuu ya kuweza kuafikiwa kwa mkataba huo kauli ilioungwa mkono naye spika wa bunge la Nairobi Beatrice Elachi.

Wakti yakijiri hayo Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi, Beatrice Elachi amesema mchakato wa Bunge la Kaunti wa kumbandua Gavana Mike Sonko utaendelea wiki ijayo jinsi ilivyopangwa licha ya gavana huyo kukabidhi majukumu yake kwa Serikali ya Kitaifa.

Akiwahutubia wanahabari muda mfupi uliopita, Elachi aidha amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuchukua udhibiti wa kaunti ya Nairobi akisema hali hiyo itafanikisha utoaji wa huduma muhimu kwa wakazi wa Nairobi kwani baadhi ya huduma hizo zilianza kuathirika tangu Sonko aliposhtakiwa.

Aidha amesema Sonko alipuuza ushauri aliopewa na bunge kuhusu mustakabali wa utendakazi wa serikali yake baada ya naibu wake kujiuzulu vilevile aliposhtakiwa. Elachi amesema Bunge la Kaunti litahakikisha sheria inazingatiwa kikamilifu katika mjadala dhidi ya Sonko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *