Wafanyakazi na mahabusu wa gereza la Kericho hio walipatikana na maradhi ya corona, sekta ya afya kaunti ya Kericho walipima sampuli 75 huku 48 wakipatikana na virusi hivyo.
Gavana wa Kericho Paul Chekwony amesema kuwa arobaini na nane hao wako katika hali njema huku waliotangamana nao wakifutwa na wizara ya afya ya kaunti hiyo.
Pia aliwauliza wakazi, marafiki na familia ya wagonjwa hao watulie na wazidi kufuata kanuni za covid-19 zilizotolewa na wizara ya afya.
Kufikia hio jana maambukizi yalikuwa yamefikia 31,441 baada ya watu 426 kupatikana na maambukizi ya corona.
Kulingana na idara ya magavana kauntii kumi na saba ambazo zina vituo vya karantini hamna mtu yeyote ambaye yuko katika vituo hivyo hii ni baada ya maambukizi kuzidi kupungua. Mwenyekiti wa magavana Wycliffe Oparanya alisema kuwa kaunti 43 ndizo zina na vituo ambavyo vinafanya kazi ya kuweka karantini huku wagonjwa 859 wakitengwa kwa ajili ya mambukizi ya virusi vya corona.
