Serikali imetakiwa kuhakikisha ya kwamba haiagizi mahindi kutoka mataifa ya nje ili kumfaidi mkulima wa hapa nchini.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha wakulima bonde la ufa Kipkorir Menjo, amesema kuwa ule mfumo serikali unaopangwa kutumia kwa sasa yafaa kuwekwa wazi kwa wakulima ili waweze kuwa na ufahamu kwa kuwa wanatarajia kupata mavuno yao hivi karibuni.
Menjo amewataka wakulima kuwa wenye subira kwa mfumo mpya ambao serikali inapania kutumia katika kununua mahindi yao.
Aidha ametoa wito kwa serikali kuweza kutoa hamasisho ya kutosha kwa wakulima wa bonde la ufa kabla ya kuukumbatia mfumo huo.