Changamoto inazidi kutolewa kwa bunge la seneti na serikali kuu kusaka mwafaka kuhusiana na mgogoro wa ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti nchini.
Viongozi wa serikali ya kaunti Baringo wakiongozwa na wawakilishi wadi pamoja na viongozi wa bunge la kaunti hiyo chini ya mwenyekiti wao Francis Koech ambaye ni karani wa bunge la kaunti hiyo amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba kaunti hazikosi fedha na hivyo kuhujumu huduma kwa wananchi kutokana na mgogoro huo.
Amemtaka rais Uhuru Kenyatta kusimama kidete na kuhakikisha ya kwamba hamna muingilio wowote wa kisiasa ila iwafaidi wananchi.