Polisi katika eneo la Malava kaunti ya Kakamega wamefunga barabara zote zinazoelekea nyumbani kwa mbunge wa eneo hilo Malulu Injendi.
Hii ni kutokana na mkutano uliotarajiwa kufanyika kati ya naibu rais William Ruto na viongozi kutoka jamii za eneo la magharibi mwa nchi.
Barabara ya Malava- Kimang’eti na ile ya Tande -Namagara ni kati ya zilizofungwa na maafisa hao wa polisi waliokita kambi katika maeneo kadha ya barabara hiyo.
Ni hatua ambayo imekashifiwa vikali na mbunge wa eneo bunge la Kwanza Ferdinand Wanyonyi.
Mbunge wa Mumuas mashariki benjamin Washiali na mwenzake wa Kimilili Didmus Barasa wamearifiwa kuzuiwa kuenelekea eneo la mkutano, huku OCPD wa malava Peter Mwanzo akifurusha Waliokuwa wamekusanyika katika boma la mbunge Injendi katika kijiji cha Lugusi kwa mkutabno huo.
Wakaazi pia wanadai kuathirika baada ya biashara zao kutatizika