Polisi aliyefutwa kazi arejeshwa na kupewa madaraka

Huduma ya polisi imemrejesha kazini afisa mmoja mkuu wa polisi  John M’mbijiwe,  aliyekuwa akihudumu katika ukanda huu wa bonde la ufa  ambaye alisimamishwa kazi kwa ajili ya sakata ya polisi Waiganjo .

M’mbijiwe sasa ameteuliwa kuwa naibu inspekta jenerali.

Katika barua  ya juni tarehe 9 , huduma ya polisi imekubali kufutilia mbali  hatua yake ya kumsimamisha kazi polisi huyo .

M’mbijiwe  alisimamishwa kazi na kushtakiwa pamoja na  Joshua Waiganjo  ambaye alishtumiwa kwa kujifanya kuwa afisa wa ngazi ya juu wa polisi  tangu mwaka wa 2012

Waiganjo  anadaiwa kusafirishwa kwa helikopta za polisi na hata alikuwa kisafiri kutumia magari ya serikali .

Alikuwa akiwaaadhibu polisi wa vyeo vya chini ,kuwahamisha wengine ,kuongoza oparesheni za polisi na hata kukagua gwaride za heshima akiwa na sare yenye nembo ya  naibu inspekta wa polisi .

Hata hivyo mwezi mei mwaka huu  mahakama ya Nakuru ilimwondolea mashtaka yote  baada ya upande wa mashtaka kukosa kuwasilisha usahidi dhidi yake . M’mbijiwe pia aliondolewa lawama baada ya mahakama kusema ushahidi uliotolewa haukutosha kuendeleza kesi yake .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *