Helikopta ya polisi yaanguka Meru

Ndege ya polisi aina ya helikopta imeanguka katika eneo la Kaithe-Kithoka, kaunti ya Meru Jumamosi, Juni 13 asubuhi.

Helikopta ya polisi ya aina ya AgustaWestland AW119 yenye usajili 5Y-NPW imeanguka katika eneo hilo Meru. Aidha kufikia sasa haijabika wazi chanzo cha ajali hio.

Walioshuhudia kisa hicho walisema ndege hiyo ilianguka ndani ya shamba la mkulima mmoja eneo hilo mwendo wa saa moja unusu mapema hii leo.

Wakti wa mkasa huo imebainika kuwa ndage hio ilikuwa na watu wanne ndani ambao walipata majeraha huku watatu kati yao wakipata majeraha madogo.

Taarifa zinadai kuwa huenda ndege hiyo ilikumbwa na hitilafu za mitambo hali iliyosababisha kuanguka. Shughuli za kutathmini idadi ya watu waliokuwa ndani zinaendelea.

Susan Kanana, mmiliki wa ardhi ambapo ndege hio ilianguka ametoa madai kuseme kuwa ndege hio ilitokomeza shamba lake lote na kuongeza kuwa ndege hio iliyokuwa ilitanda eneo hilo kabla ya kuanguka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *