Kiwanda cha kutengeneza nguo cha rivatex mjini eldoret kaunti ya uasingishu ni mojawapo ya viwanda vinavyotegemea kuwaanza kutengeneza barakoa au mask ili kuwezesha wakenya kzuia ugonjwa wa covid -19
viongozi mbambali kaunti ya uasingishu wametilia mkazo swala hilo na kusema kiwanda hicho kina uwezo wa kukamilisha shughuli hiyo kikamilifu.
Kamishina wa kaunti ya uasingishu Abdrazack Jaldesa na naibu gavana wa kaunti hii Daniel Chemno wamesema kuwa kiwa nda hicho kina uwezo wa kuitengeneza barakoa zaidi ya 3000 kila siku ambazo zitatolewa kwa wananchi kwa bei nafuu ili waweze kujikinga na maabukizi ya virusi vya corona.
Aidha wamesema ya kwamba wataendelea kutafuta msaada wa vyakula na bidhaa zingne muhimu ambazo zitaweza kuwasaidia wakaazi wa mitaa ya mabada kaunti hii.
Waliyasema hayo wakati wakipokea vifaa vya kuzuia maabukizi ya virusi hivi hatari kutoka kwa serikali kuu ambapo wamesema vitapelekwa kwa wakaazi wa mabada wasioweza kumudu bei hiyo ya bidhaa hizo.