Baadhi ya wakaazi kutoka kaunti ya uasingishu wametaka serikali kuwaruhusu wakenya kujumuika kwa pamoja katika maombi kila jumapili kwa makanisa ili kumwomba mungu awaepushe na janga la corona.
Wamesema kuwa kanisa ndio kimbilio la kila jamii katika kupata suluhisho za shida zao kila wakati. Wameelezea jinsi mikakati ya kutohudhuria kanisa imeathiri imani za wengi katika kuomba kwa pamoja huku wakisema wako tayari kuzingatia mikakati iliyowekwa na serikali ikiwemo kutokuwa kwa makundi makubwa na kuzingatia swala la usafi ili kuzuia maabukizi hayo.