Chama cha walimu cha KNUT tawi la Uasin Gishu linataka serikali kuweka sera za kudumu kuhakikisha kwamba bima ya afya ya jamii SHA inafanya kazi ipasavyo la sivyo nia yao ya mgomo bado ungalipo.
wakizungumza kwenye mkao na wanahabari jijini Eldoret,walimu hao wakiongozwa na John Koech ambaye ni mwenyekiti wa KNUT Kanda la Rift Valley ,walimu hao wanasema baada ya kufanya mkutano na wasimamizi wa SHA katika Kunti hiyo ya Uasin Gishu wanatarajia matakwa yao yataangaziwa.
Walimu hao wanasema wanahisi kuna baadhi ya maafisa kwenye sekta ya SHA ambao wanajaribu kuhitilafiana na shughuli za walimu wakitaka tume ya kuangazia huduma za walimu nchini TSC kuwa macho na kuweka kipaumbele matakawa ya wafanyikazi wake.
yanajiri haya,wakati walimu hao walikuwa wametishia kulemaza shughuli za masomo pindi tu shule zitakapofunguliwa jumattu juma lijalo,ila kutokana na mazungumzo hayo,wazazi wanasubiri iwapo wataendelea na shughuli hiyo ama watasubiri matakwa waliyowasilisha mapema leo Jumatano kushughulikiwa.
