Askofu wa Jimbo katoliki la Embu Peter Kimani ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kumpa aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga heshima kwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.
askofu Kimani amesema kuwa taifa linaweza tu kusonga mbele ikiwa viongozi watajitwika jukumu la kutekeleza yale ambayo hayati Raila alikuwa akipigania kama vile usawa kwa watu wote vita dhidi ya ufisadi, akisema kuwa njia ya kumshukuru kiongozi huyo siyo sifa kutoka kinywani mwa wanasiasa bali yawe kwa matendo.
amesema kuwa taifa la kenya linajivunia mambo mengi kutokana na juhudi zake za kuleta mageuzi nchini na endapo juhudi hizo zitawekwa pembeni huenda taifa litarudi nyuma hatua kadhaa tofauti na ilivyokuwa ndoto zake
