Wito umetolewa kwa familia kuwapokea vyema watumishi katika shamba la bwana ili waweze kutekeleza jukumu lao kwa njia inayostahili.
Askofu wa jimbo la Jeshi Wallace Ng’anga’ alisema kwamba wakati mwingi watumishi hao hupitia hali ngumu kutokana na kile anasema kutopata uungwaji mkono kutoka kwa familia zao swala analosema kwa muda huenda ikahujumu shughuli za uenezaji wa injili.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya kanali Dancun Ndegwa huko Hurligham Nairobi,askofu familia ni kiungo muhimu ya kukuza miito mbali mbali na iwapo makleri na majandokasisi hawatopokea uungawaji mkono wataishia wakiangaika kwenye utume wao.
Aidha,askofu Wallace alisisitiza haja ya kila mkristu kutambua kuwa japo ukristu huja na changamoto si haba wasije wakakata tamaa kwa kuwa mwenyezi mungu huwaongoza kila muda.