Uasin Gishu; Corona Yaathiri Sekta ya Mitumba.

Kufuatia mkurupuko na maambukizi ya virusi vya corona nchini Kenya wauzaji wa nguo za mitumba mjini eldoret kaunti ya uasin gishu wameathirika zaidi katika sekta ya biashara.

 Wakielezea wasiwasi wao wamesema kuwa janga hili limefanya hawapati wateja kama ilivyokuwa hapo awali kabla  ya virusi hivi kuingia nchini.

Wamesema kuwa wateja wengi  wamesalia nyumbani wakihofia maabukizi hayo na hivyo hawana kuwauzia nguo hizo.

 Hata hivyo wanakadiria hasara kubwa ikizingatiwa kwamba hawapati mizigo kwa vile hawasafiri kuleta kwa bei inayofaa na na wanapata hata wakati mgumu kulipa kodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *