Kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom kwa sasa imeondoa ada ambayo inatozwa kwa wateja wake wanaotima pesa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine kwa wale wanaotumia kiwango cha chini ya shilingi 1000.
Safaricom vilevile imeongeza kiwango cha fedha zinazoweza kutumwa kwa siku kutoka shilingi elfu sabini hadi shilingi elfu mia moja hamsini.
Haya yanajiri baada ya agizo kutoka kwenye benki kuu ya CBK kwa kutaka benki zote kuondoa ada hizo kwa shilingi elfu moja kwenda chini.
CBK wakati huo imeelezea kuwa hatua inalenga kuwasaidia wakenya zaidi kulipia huduma na bidhaa tofauti kwa kutumia kwa kutumia rununu na kujizuia kutumia pesa taslimu ili kuzuia kueneo kwa virusi vya korona.
Vilevile CBK imesema kuwa itafuatilia kuhakikisha kuwa utekelezaji wa agizo hilo kwa siku tisini zijazo