“Hatuendi Uganda na Rwanda”, Jambo Jet yasema

Kampuni ya ndege ya Jambo Jet imesitisha safari zake kuelekea mataifa ya Uganda na Rwanda kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya Corona.

Hatua hii inajiri baada ya safari zote za ndege kuelekea mataifa yaliyoathiriwa kupigwa marufuku kufuatia agizo la rais Uhuru Kenyatta. Nchini Rwanda, maambukizi ya virusi hivyo yamefikia watu saba huku Tanzania ikiripoti kisa kimoja nayo Uganda ikiwa bila ya kisa chochote kufikia sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *