Kutubu maisha freshy

Askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi David Kamau amewataka wakristu kuwa na hulka ya kukiri makosa yao na kuishi maisha ya sakramenti ili kuurithi ufalme wa mbingu.

Akihubiri katika misa ya kila mwaka ya kikundi cha MYM askofu Kamau amesema kuwa ndoa nyingi husambaratika kwa sababu ya kila mmoja katika ndoa hiyo kutokubali kukiri makosa yao.

Askofu kadhalika aliwaonya wale wanaoshiriki matendo ya ufisadi kushiriki sakramenti ya kitubio kabla ya kushiriki meza ya Bwana akisema kuwa kule kuchanganya ufisadi na ekaristia ni tendo la dhihaka kwa mwenyezi Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *