Wanachama wa chama cha United Democratic Alliance UDA kaunti ya Uasin Gishu wameonekana kuunga mkono matozo ya ushuru kwa kile wanasema ni kusaidia taifa kusimama na kuiwekea taifa msingi dhabiti kwa miaka zijazo.
Wakiongozwa na mbunge wa Turbo Janet Sitienei wanasema kwamba wakenya wataweza kufurahia matunda ya ushuru huo kwa miaka zijazo na kuwataka kuunga mkono serikali kwa shughuli zake.
Aidha,wanachama hao walisema kwamba wanaamini kwamba japo taifa linajikokota kutokana na gharama ya maisha,taifa litarejelea kwenye njia mwafaka hivi karibuni.