Mkunje samaki angali mdogo

Askofu mstaafu wa jimbo katoliki la Kitale Maurice Anthony Crowley ametoa wito kwa shule mbalimbali kuwa na umoja na kumtanguliza mwenyezi Mungu kama njia moja ya kuafikia mafanikio.

Akihubiri katika Misa ya kikundi cha vijana alamarufu YCS, askofu Crowley alitoa wito wa ushirikiano baina ya walimu na wanafunzi akisema kuwa ushirikiano huo ndio utakaofanikisha ruwaza na malengo ya shule.

Askofu Crowley ametoa wito kwa Kila mwanafunzi kujivunia shule na masomo akisema kuwa mafanikio huja kwa kupenda masomo ndio njia ya kipekee ya kufaulu katika maisha Yao.

Aliwataka wanafunzi kuwa Wacha Mungu kwa kutekeleza mapenzi ya Mungu akisema kile kinatekelezwa bila uwepo wa mwenyezi Mungu ni sampuli ya mbegu mbaya iliyoanguka kwenye mawe.

Alishutumu visa vya mauaji dhidi ya watoto katika mataifa mbalimbali akisema kuwa wanachochewa na hila za kishetani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *