Jimbo kuu katoliki la Nairobi imezindua mbinu mkakati wa kuwajenga kiimani waumini wachanga na ambao wanaendelea na masomo yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambao pia ulikuwa siku kuu ya walimu katika jimbo kuu hilo,askofu mkuu wa jimbo hilo Philip Anyolo Subira amewataka walimu kuwa chombo kuu cha kuinua na kujenga ukristu kwa wanafunzi hao,akisema kizazi kichanga kikipata kumtambua mwenyezi mungu kitasimama imara na kusaidia jamii kwa maswala mazuri na ya kutia moyo.
Aidha,askofu mkuu Anyolo aliweka wazi mbinu mkakati hizo akiwataka wanajimbo kuunga mkono ili iweze kufanikiwa.