Ipo haja ya wakazi katika bonde la Kerio Kuunga mikono kupambana na jinamizi la utovu wa usalama na uhalifu katika eneo hilo.
Akizungumza katika eneo la Kinyach mpakani mwa Kaunti za Elgeyo-Marakwet na Baringo,askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich alisema yawapasa wakaazi eneo hilo kuwa mstari wa mbele kupiga vita ugaidi huo kwani wao wenyewe wanayouwezo wa kuitokomeza.
Wakati huo,askofu Kimengich aliwataka wakuu wa serikali za kaunti zinazopakana Kerio Valley kuweka mikakati ya miradi ya maendeleo ndipo vijana na wakazi kwa jumla wapate kuajiriwa na uhalifu kumalizwa.
