Ujasiri kueneza injili

Wakristu wametakiwa kuwa na ujasiri katika uinjilishaji licha ya changamoto wanazopitia maishani mwao.

Akihubiri katika  kathedrali ya mtakatifu Teresa Kibuye jimbo kuu katoliki la Kisumu, askofu mkuu wa jimbo hilo Maurice Muhatia Makumba amesema kuwa kamwe mkristu asiyumbishwe kiimani na yale magumu anayopitia maishani mwake, iwe katika sehemu ya kazi au mahali popote pale.

Alitoa wito kwa kila moja kutia ujasiri katika harakati ya uinjilishaji, akisema kuwa changamoto ambayo humwandama mkristu katika zoezi hilo ndio itakayomtia nguvu na uwezo wa kukabiliana nazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *