Nani Alimuua Sgt. Kenei?

Wafanyikazi wanne katika afisi ya naibu wa rais William Ruto wanatarajiwa kuhojiwa hii leo kufuatia kifo cha sajenti Kipyegon Kenei.

Maafisa wa idara ya upelelezi DCI pia watawahoji wafanyikazi wawili wa kampuni moja ya mawasiliano na watatu kutoka idara ya jeshi.

Washukiwa hao wanahusishwa na mauaji ya Kenei takriban wiki mbili zilizopita kufuatia uchunguzi uliofanyiwa mawasiliano ya simu ya mwisho kabla ya kifo chake.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, maafisa wawili wa jeshi walikuwa na mawasiliano na mmoja wa washukiwa kwa jina Daniel Otieno Omondi.

Miongoni mwa wafanyikazi wanaotarajiwa kuhojiwa na DCI ni mmoja ambaye inadaiwa kuwa Kenei alimpigia simu akiomba ushauri wa jinsi ya kuandikisha taarifa mbele ya DCI kwani tayari alitarajiwa kuhojiwa.

Mshukiwa mkuu katika sakata ya zabuni ghushi ya vifaa vya kijeshi vya gharama ya Sh.39bn Rashidi Echesa aliachiliwa huru na mahakama kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *