Hatimaye Mbunge wa Msambweni, Suleiman Dori amezikwa kijijini kwao Gazi kwenye Kaunti ya Kwale hii leo.
Hafla hio ya mazishi yake mbunge huyo ilihudhuriwa ndugu, jamaa na marafiki walitumia muda huo kutuma salamu na kumsifu marehemu kwa uongozi bora.
Dori amefariki asubuhi ya kuamkia leo alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Aga Khan, Mombasa kufuatia maradhi ya saratani.Inasemekana kuwa mbunge huyu amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi ikiwa ni kwa mujibu wa familia.
Mbunge huyo ametajwa kuwasilishwa hospitalini hio jana jioni baada ya kupata shinikizo la damu na kupelekea kulazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kufariki mapema hii leo.
Itakumbukwa kuwa Suleimani Dori alichaguliwa kwa muhula wa pili kuwa mbunge kupitia tiketi ya chama cha ODM mwaka wa 2017 wakti huo akiwa ni mwenyekiti wa wabunge kutoka pwani. Dori sasa ni mmoja wa viongozi kadhaa waliofariki dunia miaka ya karibuni kufuatia maradhi ya saratani wakiwa ofisini. Nao ni aliyekuwa Gavana wa Bomet Joyce Laboso, Mbunge wa Kibra Ken Okoth, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom, Michael Joseph miongoni mwa wengine.