Toba na Wongofu ni safari ya Mbinguni

Kanisa linapoadhimisha kipindi cha toba sala na matendo ta kiutu almaarufu kwaresima wakristu wametakiwa kujirudia kwa kutafakari safari ya ukombozi msalabani.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Subira Anyolo amesema kuwa huu ni wakati ambapo kila mmoja anastahili kuweka agano dhabiti na mmweneyzi Mungu kwa kujisalimisha kwake kristu kupitia kwa sala toba na halkadhalika kutenda matendo ya kiutu akisema kuwa agano kati ya mja na muumba wake hupyaisha na kubadilisha maisha hayo.

Amewataka wakristu kadhalika kutupa utu wa kale na kuomba radhi kutoka kwa mwenyezi Mungu akisema kuwa penye msamaha pana njia na penye msamaha huo kuna uponyaji ambao huondoa utu huo wa kale.

Askofu mkuu huyo kadhalika ametoa wito wa kukomeshwa kwa mafarakano kati ya ndugu na ndugu akisema kuwa kipindi hiki kinatoa nafasi ya maridhiano na mshikamano wa kila familia jambo ambalo anasema kuwa linaweza tu kuafikiwa kupitia sala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *