Askofu wa jimbo katoliki la Kakamega Joseph Obanyi Sagwe alipongeza hatua ambayo kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amechukua kuwania wadhifa wa uenyekiti kwenye tume ya Afrika AUC akisema kwamba hilo ni jukumu jipya na la Kipekee.
Akizungumza mjini Eldoret,askofu huyo alisema kwamba kiongozi huyo amekua mwenye bidii na fursa hii itamewasadia wakenya wengi kujifunza kwake.
Askofu Sagwe alitupuuzilia mbali dhana kwamba iwapo Odinga atajiunga na tume hiyo upinzani utazorota akieleza kwamba kutokana na uongozi wake kwa miaka mingi kuna matumaini kwamba wapo baadhi ya viongozi wa upinzani waliowekewa msingi imara.
Askofu Obanyi alitumia fursa hiyo kuwataka wakristu kulinda checmichemi za maji na kutumia vyema maji katika makaazi yao,kanisa katoliki likiingia wikiyake ya pili kwenye msimu wa Kwaresma.
