Umakini kwa upatikanaji wa amani

Wenyeji katika bonde la Kerio wakiendelea kukabiliwa na utovu wa usalama,wito umetolewa kwa asasi za kiusalama ishirikishe umma ikiwa ni wakaazi,viongozi wa kidini na washikdau mbalimbali kutokomeza hulka hiyo.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich alisema kwamba inasikitisha kwa wenyeji kuendelea kuishi kwa hofu ilhali serikali imekua na msimamo wa kukabiliana na utovu akisema ushirikiano ndiyo nguzo muhimu kwa sasa.

Yanajiri haya huku wakaazi kaunti zinazopakana katika bonde la kerio hasa kaunti ya Baringo wakihama makaazi yao kufuatia kuwauwa kwa wanafunzi wawili siku ya jumatatu kutoka shule ya msingi ya Yatya,shule takriban saba kwa sasa zikiwa zimefungwa.

Askofu Kimengich kadhalika,alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi kuwa karibu na wanao msimu huu wa likizo fupi ili wasijeze wakajiingiza kwenye vikundi visivyostahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *