Hakuna mtimilifu

Askofu mteule wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Monsinyo Simon Peter Kamomoe amewataka wakristu kujiepusha na hulka ya kuwahukumu wale wanaoteleza na badala yake wawatendee matendo ya huruma .

Akihubiri katika kanisa la Holy family Basilica Jijin Nairobi askofu mteule monsinyo Simon Peter Kamomoe amewataka wakristu siku zote kuinga mfano wa Mungu kwa kutenda matendo ya huruma akisema kuwa hulka ya kuwahukumu watenda dhambi kupitia ndimi ni dhambi ambayo itamnyima mkristu kuurithi ufalme wa mbingu.

Ametoa wito wa mshikamano katika familia mbalimbali akisema kuwa kule kulaumiana katika familia huweka familia nyingi katika hali ya mafarakano ambayo hatimaye hutenga familia hizo.

Mteule huyo ametoa wito kwa wanandoa kutafakari thamani ya ndoa huyo na kuanza kuitafakari kama sakramenti ambayo inastahili kudumishwa kama njia moja ya kudhihirisha upendo wa Mungu.

Ametaja hulka ya kutosamehe kama kushikwa mateka na shetani akisema kuwa penye msamaha pana njia na penye msamaha na furaha akitoa wito kwa wakristu kadhalika kuwa na mazoea ya kushiriki toba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *