Baba mtakatifu Francisko amewateua maaskofu wasaidizi wawili katika jimbo kuu katoliki la Nairobi.
Katika tangazo ambalo limetolewa na mwakilishi wa Baba mtakatifu hapa nchini na Sudan Kusini Mathews Hurbatus van Megen kwenye misa ya saa saba mchana majira ya Afrika Mashariki katika Basilica ndogo jijini Nairobi Mwadhama Hurbetus amewatangaza padre Simon Peter Kamomoe na padre Wallace Ng’ang’a.
Padre Peter Kamomoe hadi kuteuliwa kwake amekuwa msimamizi wa kathdrali ya Holy Familiy Basilica jijini Naiobi huku padre Wallace Nganga akihudumu kama mshirikishi wa idara ya kipastorali jimbo kuu katoliki la Nairobi na paroko wa wa parokia ya Malkia wa Mitume Ruaraka hii hapa ni mwakilishi wa Baba Mtakatifu Hurbetus Van Megen.
Wateule hao wawili ni mapadre wa jimbo kuu katoliki la Nairobi, Wateule hao sasa watakuwa na jukumu la kusaidia askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki Philip Subira Anyolo katika shughuli za jimbo kuu hilo.
hii itakuwa ni mara ya pili kwa baba mtakatifu kuwateua maaskofu wawili kutoka jimbo kuu katoliki la Nairobi kwa wakati moja.
Ikumbukwe kuwa uteuzi sawia na huu ulikuwa mwaka wa 1999 ambapo askofu David Kamau na askofu Anthony Ireri Mukobo kutoka jimbo kuu katoliki la Nairobi waliteuliwa kuwa maaskofu wasaidizi.
Askofu David Kamau aliteuliwa kuwa askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Niarobi huku askofu Ireri Mukobo akiteuliwa kuongoza Vicarieti ya Isiolo.
Akikiaribisha uteuzi huo askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Niarobi Philip Anyolo amseshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kuridhia ombi hilo akisema kuwa wawili hao watashirikisha kikamilifu uenezwaji wa injili katika jimbo kuu hilo.