WATEULE WAAPISHWA

Bunge la kaunti ya Uasin Gishu limewaapisha waakilishi wadi wateule 13 ambao majina yao yalichapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali.

Akiongoza vikao hivyo,spika wa bunge hilo Philip Muigei amesema kwamba wawakilishi hao watanza rasmi shughuli zao za kuwashughulikia wakaazi.

wawakilishi hao wateule ni pamoja na mwakilishi wa watu wanaoishi na changamoto za Kimaumbele miongoni mwa wawakilishi wa vikundi mbalimbali.

bunge hilo sasa liko tayari kurejelea shughuli zake za kawaida baada ya kuteuliwa kwa wawakilishi hao ambao wanaafikia  viwango vinavyohitajika kisheria.

yanajiri haya baada ya hapo awali mahakama ya  kuu ilivunjilia mbali vikao vyote vya bunge hilo kwa madai kuwa vilikuwa kinyume cha sheria kwa uteuzi wa wawakilishi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *