Waumini wametakiwa kuweka hazina yao Mbinguni kwa kujenga kanisa ambayo ni msingi ya imani ya kila mkristu.
Askofu wa jimbo katoliki la Meru Selasius Mogambi amewataka waumini siku zote kushiriki katika ujenzi wa kanisa akisema kuwa kanisa ndia mahalia inayowaunganisha wana wa Mungu kwa umoja akisema kuwa umoja huo una matunda mengi ambayo utapelekea mkristu kuurithi ufalme wa mbingu.
Askofu huyo kadhalika amewataka waumini wote siku kuonyesha heshima kama inavyohitajika kiliturjia kwa kuvaa mavazi ya heshima kwa kuwa siku zote yu hai katika tabernakulo na kule kutoonyesha heshima kanisani kutokana na hulka hiyo ya kutovaa vyema huonyesha dharau na chukizo kwa mwenyezi Mungu.
Ametoa wito kwa wale wanaonuia kuendeleza mikutano ambayo si ya kueneza injili kutofanya hivyo katika sehemu za maabadi akisea kuwa kadhalika yanaonyesha dharau