Familia zimetakiwa kusali pamoja na kuishi kwa upendo kwa faida ya mshikamano wa familia kwa kuwa familia ndio chimbuko ya miito mbalimbali katika kanisa.
Askofu wa jimbo katoliki la Kakamega Joseph Obanyi Sagwe akihubiri katika misa ya shukrani ya kusherehekea miaka ishirini na tano ya mtawa Nancy Mbae eneo la Chuka jimbo katoliki la Meru askofu Obanyi amesema kuwa familia nyingi zimekumbwa na misukosuko akitoa wito kwa familia kuombeana kwa faida ya umoja wa familia hizo anayosema ni chumbuko la miito mbalimbali.
Amewataka watawa na wale wanaofanya kazi katika shamba la bwana kumtegemea mwenyezi Mungu kila siku akisema kuwa maisha hayo yana mawimbi mengi ambayo inahitaji tu wanyenyekevu na waliodhabiti katika imani.
Askofu huyo ametoa wito kwa wazazi kujaza nafasi ya kuwaelekeza watoto kwa kuwa wengi huvutiwa na mambo mengi maovo akitoa wito kwa vijana nao kuwa na hulka ya kuskiliza wazazi wao.
