Uwajibikaji kwa wakuu wa gatuzi

Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu katika kaunti ya Uasin Gishu wanatoa pendekezo kwa Rais William Ruto kubuni jopo litakalo simamia uangalizi wa utendakazi wa magavana nchini ili kupunguza ufujaji wa mali ya umma.

Wakiongozwa na afisa mkurugenzi wa shirika la Center for Human Rights and Democracy Kipkorir Nge’tich ni kwamba baadhi ya magavana wanahujumu shughuli ya maendeleo kwa kujiingiza kwa ulafi huo ambao wanasema haistahili na sharti lichunguzwe.

Nge’tich alisema kwamba uwepo wa jopo hilo litasaidia pakubwa kwa kuwaweka kwenye ramani magavana na kwa wao kuwajibikia utendakazi wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *