Viongozi wa kidini Nchini waniataka jamii kuwahamasisha wavulana na wasichana ili waweze kuishi kwa amani na kupunguza visa vinavyohusiana na dhulma za kijinsia.
Wakiongozwa na askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini Jackson Ole Sapit,viongozi hao walisema kwamba visa vya mauaji yanayotokana na Dhulma za kijinsia zimekithiri mno swala ambalo lisipoangaziwa kwa hivi karibuni litawaangamiza vizazi vijavyo.
Viongozi hao walisema kwamba kwa sasa jamii si salama kwani zaidi ya watu 159 wameripotiwa kuwaua kuanzia Octoba mwaka jana hadi mwezi huu jambo ambalo wametilia shaka. Wakati huo viongozi hao wamaitaka serikali kutekeleza sheria na sera za kukabiliana na dhulma ya kijinsia.