Hifadi mazao

Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika eneo la Lelan, Kaunti ndogo ya Marakwet Magharibi, kaunti ya Elgeyo marakwet, wametakiwa kuhifadhi masalio ya mazao kama chakula cha mifugo.

Haya ni kwa mujibu wa Elijah Keter, afisa kutoka kampuni ya maziwa ya Brookside ambaye aLIsema kuwa ni muhimu kwa wafugaji hao kuanza kuweka hifadhi ya kutosha ya chakula kwa mifugo wao ili kuepuka uhaba wa biadhaa hiyo wakati wa kiangazi.

Akiongea katika eneo la Lelan, afisa huyo aLIsema kuwa kampuni hiyo itawapa mafunzo wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kuhusu mbinu bora za kilimo ili kuimarisha mapato yao katika sekta hiyo.

Wakati uo huo, aLIwashauri wakulima kutoka eneo hilo kukumbatia upanzi wa miti kupiga jeki juhudi za serikali katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *