Polisi Mjini Eldoret waliwanasa watu sita wanaoaminika kuendeleza biashara haramu ya mihadarati.
Akithibitisha haya,kamanda wa polisi kaunti hii Benjamin Mwanthi amesema kufuatia oparationi iliyoongozwa na maafisa wa usalama kwa ushirikiano na maafisa wa kupambana na mihadarati na kwamba watu hao walipatikana na aina mbali mbali ya vileo na hata bangi nyuma ya jengo ambalo halikukua limekamilika.
Wakati huo kamanda aliwataka wakaazi kuendelea kutoa ripoti kwa polisi kuhusu wafanyibiashara ambao wanaendeleza biashara isiyo halali ili kupambana na biashara hiyo.