Serikali imetakiwa kuhakikisha kuwa kuna ugavi sawa wa rasilimali kwa wakaazi wanoishi katika mipaka ya kaunti ya Elegeiyo Marakwet na Pokot magharibi.
Akihubiri kwenye hafla ya maombi ya madhehebu mbalimbali iliyoandaliwa mjini Iten na kuhudhuriwa na rais William Ruto pamoja na viongozi wengine askofu kimengich alisema kuwa swala kuu linalopelekea maafa mingi katika eneo hilo la bonde la Kerio na ukosefu wa ugavi sawa wa rasilimali.
Askofu Kimengich ametoa wito kwa serikali na asai husika kuhakikisha kuwa jinamizi la ufisadi linakabiliwa akisema kuwa na swala ambalo limepelekea wakenya wengi kusalia kwenye lindi la umaskini.
Aliwataka wakaazi katika maeneo hayo pamoja na wazee na jamii kwa ujumla kujitokeza na kuhubiri amani katika eneo hili ili wakaazi hao wafurahie matunda ya amani.