Tumieni msimu wa mvua nyingi kupanda miti

Wakazi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wamehimizwa kutumia msimu huu wa mvua kupanda mimea inayochukua muda mfupi kukomaa.

Akiongea katika eneo la Kapsowar gavana wa kaunti hiyo Wesely Rotich, alisema hatua hiyo itasaidia kuwepo kwa chakula cha kutosha katika kaunti hiyo.

Rotich aliwataka wakazi kukuza mimea kama vile Viazi, maharagwe, Viazi vitamu na aina mbalimbali ya mboga kujitosheleza kwa chakula kadhalika, kupata mapato ya ziada.

Aidha gavana huyo amewataka wakazi kutumia maji kwa njia inayofaa na pia kuhifadhi maji hayo kwa matumizi ya siku za baadaye wakati wa ukame.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *