Kuweni mabalozi wema mitandaoni

Vijana wametakiwa kuwa mabalozi wa kristu kwa kutumia mitandao ya kijamii ili kueneza habari njema ya ufalme wa mbingu  kwa dunia nzima.

Haya ni kwa mujibu wa askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ambaye anawakilisha baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB kwenye kongamano la sinodi linaloendelea mjini Vatican, akisema kuwa vijana wengi wanatumia mitandao ya kijamii kwa asilimia kubwa akiwataka kujiepusha na maswala yanayokinzana na maadili na badala yake watummie majukwaa hayo ili kueneza habari njema ya kristu kwa dunia nzima.

Ametoa wito kwa vijana kujitokeza waziwazi na kwa ujasiri kukiri imani yao kwa kristu kwa kuwa hiyo ndio njia ya kipekee ya kuhakikisha kuwa kanisa mahalia nyumba ya wote linasalia imara  hata katika kizazi kijacho.

Amaesema kuwa kongamano la sinodi linaloendelea mjini Vatican limeipa kipaumbele maswala yanayohusu vijana na chanagamoto zao sindodi ikiwa inahusu ushirikishwaji na kutembea pamoja kama njia moja ya kujenga na kuinua kanisa mahalia nyumba ya wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *